Goodboy

Advocating For Change

Elimu Ni Ngao ya maisha November 1, 2008

Filed under: Uncategorized — petermwatha @ 10:55 am
Tags: , , , ,

Elimu ni ngao ya maisha, ni  muhimu sana kwa sababu kama mtu hajasoma ni vigumu aweze kuajiriwa.

Mfano ni kwamba, mtu akizuru mitaa mengi, ni jambo la kuhuzunisha kupata vijana wengi wakizurura na kupiga gumzo usio na manufaa hata kidogo. Sio kwasababu, hawana la kufanya, ni kwa vile hawakupata fursa ya kuhitimu masomo na pia wavyele wao hawakutia maanani kuwafunza.

Hata hivyo, kuna mabwenyenye wanaowatumia watoto kwa manufaa zao za ubinafsi, kama vile, kuwabebesha takataka, kuwaambia watafute vitu kama vyuma vya biashara zao ilhali malipo ni duni kabisa.Ni matatizo kama haya yanayowakumba na kuwafanya vijana watoroke nyumbani mwao.

Sio tu kazi ya utumwa, inasababisha  vijana kutoroka makwao, pia utumiaji wa dawa ya kulevya imechangia pakubwa. Wanavyo meza tembe zisizo halali kwa wingi, wengi wao huanza kushiriki katika wizi, iliwaweze kununua hizo dawa na kujikimu kiafya.

Nasisitiza zaidi hili hoja ya,” umuhimu wa masomo,” kwa vile wendani wangu wa kufa na kupotea, waliaga dunia mwaka wa 2006, kutokana na uhalifu tuliokuwa tumezoea kutekeleza ikawa mazoea.

Tulikuwa waporaji mali za watu kwa kuwanyonga na hata kuwajeruhi vibaya sana ili tu , tuweze kuwanyanganya mali zao. Lakini, baada ya wenzangu kufyatuliwa risasi na polisi, niliamua kubadilika, kwa kujitegemea kibinafsi bila ya kuwanyanganya watu vitu vyao.

Sina budi, ila tu kuwashukuru watu wa Undugu Society of Kenya, kwa vile wamejimudu na kujikakamua vilivyo kuyashughulikia mahitaji ya watoto wasiojiweza, sio tu kimaumbile, bali pia kwa kuwapa fursa ya kupata elimu.

Wengi wetu tulikuwa chokoraa kama vile tunavyotambulikana katika miji. Lakini, undugu imetushughulikia vilivyo maishani, kwa sasa, sisi ni sawa na watoto wengine, wawe wa mabwenyenye, bado tuko sawa kimasomo.

Ni tumaini letu ya kwamba, ndoto zetu za maishani zitakuja kuona mwangaza siku za usoni.

Translation

Knowledge is power!

Education is very important because if you are not educated you cannot be employed anywhere. If you walk on the streets you will find many youths who are not educated and others did not complete their education, as a result of parents negligence.

It has become a heavy task for us to get worthwhile jobs, forcing most of us to get involved in shoddy businesses, making us be the slaves of the rich people who end up misusing us for their own selfish benefits

There are those people who mistreat us, by giving us hard tasks to perform, like collecting garbage and collecting plastic containers for recycling purposes. They pay us peanuts, and end up selling the items five times what they pay us.

If we complain, they threaten to throw us in jail or even to stop buying the items from us. Yet they are aware that the little cash they give us is not enough to cater for our daily needs.

More so, drugs has ended up killing the dream of education among the youths. This habit made us steal to an extent of even using violence, so that we could cash in money to go and buy with drugs. We became a public enemy. No one so the need to assist us as a result of our bad behavior.

All in all, a friend in need came, one who could understand us, related with us, was ready to transform our lives to the better.

Without the help of Undugu Society of Kenya, most of the street children would have never ever lived to see the dream of change in their lives.

U ndugu has made us great and we are proud of it, for they have enabled us acquire basic education for free, thus, making us be self reliant. Academically, we can stand on the same platform with children from rich families, a great idea that we never imagined to ever acquire in life.

.


 

Umasikini Kwa Wingi July 29, 2008

Filed under: Uncategorized — petermwatha @ 2:21 pm
Tags: , ,

Umasikini ulitoka kuwa watu weigine kujinyakulia viwaja mingi.

Weigine hawana mama wala baba wakutegemea. Inabidi waende kwa mtaa kuomba viakula. Ukitembea asa vijiji bali bali hutapata watu hawajiwezi vilema inabidi waede toun kuomba pesa za kununua chakula na zalipa nyumba. Ukipata vijana wegi kwa mtaa watakupatia shida bali bali kama wazazi kufaliki madawa za kulevwa kuwalibu na kukosa kazi.

Umasikini unatuma wasichana wegi wanajiushisha na usharati kwa sababu wanaona tabia za wazazi wao. Weigine kujiushisha na usharati kukunywa pombe za bei lahisi weigine wali poteza mali zao siku za uchaguzi asa kuchomewa mali zao kubomolewa plot zao na kunyaganywa vitu za nyumba. Pia kuna wale wali poteza wazazi wao siku hiyo ya uchaguzi nigeomba kama hawa watu wanaweza kusaidiwa na serikali. Kama vijana wapewe kazi ama muradi ile wanaweza KUJISAIDIA NAZO.

Translation

Poverty

Poverty originated in Kenya when people took large portions of land in the past.

Many of these poor people are orphans so they have no one to depend on. This has led them to be street children and beg for food. When you take a walk in different neighborhoods, you see disabled people who can’t take care of themselves so they are forced to go to town to beg for money to buy food and pay rent. When you meet the youth in the streets, they will tell you the different problems they face like the death of their parents, drug abuse and their lack of job opportunities.

Poverty has led many girls to prostitution, due to the difficulties of their parents. Most of them joined prostitution and started drinking cheap alcohol. During the post election violence, many people lost their properties because of arson, demolition and robbery. Also, some people lost their parents that day. I would request that the Government assists those who lost their parents during this time. For instance, the government could give the youth job opportunities, education or training so the youth can benefit.