Goodboy

Advocating For Change

Mbona hili kero? July 16, 2008

Filed under: Uncategorized — petermwatha @ 7:29 am
Tags: , , , ,

Tangu zama za zama, wananchi wa Kenya wamekuwa wakihangaishwa na idara ya polisi bila sababu mwafaka.

Hasaa, vijana,na jambo hili limekuwa kero kubwa kwetu sisi,kisa na maana, hakuna usalama wa kutosha na pia huru. Ilhali, hizi mbili ni haki zetu.

juzi,baada ya kazi sulubu,ilikuwa sabalkheri,ambapo tuliamua kupiga gumzo huko mtaani, huku tukipumzika. Baada ya nusu saa,tuliona gari ya buluu ikiendeshwa kwa kasi,muda sio muda,ilitukaribia na polisi waliokuwa wamejiami kwa bunduki wakaja tulimokuwa tumekaa.

Sawia, walituamuru tutoe vitambulisho vyetu. Baada ya kuvikaguwa, tuliamrioshwa kulala chini kwa tumbo,ambao ulikuwa sawa na kubusu ardhi. Walipekua mifuko yetu,wakidai ya kwamba walikuwa wanatafuta dawa ya kulevya.

Tulipoamrishwa tusimame,tupande hilo gari ya polisi,tulipigwa na butwaa na kubaki tumebungáa. Cha kushangaza zaidi,hatukuwa tumetekeleza uhalifu, pili, hatukuwa na dawa ya kulevya, tatu,hatukuwa wezi. Ni sababu gani tulikuwa tunatiwa pingu?

Waliindesha hilo gari kwa mwendo wa kasi,na tulipofika katika kituo cha polisi,tuliamriwa  tutoe viatu pande moja,na tulipowauliza ni sababu gani tulikuwa tumekamatwa? walianza kutushambulia kwa mateke na ngumi, huku wanatuita mahabusu wasiop na nidhamu.

Tulifungiwa kwenye chumba cha mahabusu. Humo ndani, kulikuwa na giza totooro,kujitambua kukawa sawa na kutega kitendawili.Ingawa tulikuwa mahala moja,mtu kutambua mwenzake ilikuwa kazi sulubu. Meno tu, ndizo zilikuwa zinaonekana.

Tulipofikishwa korokoroni, tulishtakiwa kwa maadai kwamba sisi tulikuwa  washiriki wa kundi haramu ya Mungiki. Kwa hivyo, iliwabidi watukamate kwa vile tulikuwa hatari kubwa kwa usalama wa wananchi.

Tulijaribu kujitetea kwa vilivyo, lakini vilio vyetu vilimwagikia patupu.Hakimu alipotoa maoni yake, aliamuru tufungwe kwa muda wa miezi mitano,ili tuweze pata mdaa wa kubadilika,ili tuweze kuishi kwa usalama na jamii zinginezo.

Ijapokuwa, tulikerwa zaidi, hatukuwa na la kufanya. Machozi ya uchungu yaliteremka machoni mwetu,lakini,tayari,jambo ilikuwa imeshatekelezwa.

Hivi ndivyo serfikali inafaa kuwahudumia wananchi?

Tulipelekwa jela kwa muda wa miezi tano na tulivumilia hadi tukaachiliwa. Hutuelewi jinsi ya kutatua hii shida kwa sababu bado wanatusumbua tukiwa zaidi ya watu ishirini na tano ama watu kumi. Ningeomba kama tunaweza kusaidiwa ili serikali iwache kutuhangaisha.

Translation

Police Harassment

Police harassment at our base is so much that we cannot conduct peaceful gatherings. The police come chasing us for no reason. While we are working, we wear soiled clothes to avoid messing up our better clothes. This triggers police humiliation as they claim we are thieves despite constantly informing them that we are just street children.

For instance, one day as we relaxed near a shamble kiosk at around eight o’clock, we saw a vehicle driven towards where we were. We did not imagine they were our guests until the vehicle parked just next to us. To our surprise, we were given matching orders to all get into the vehicle. We found ourselves at the police station. To add insult to injury, we were charged with belonging to the outlawed ‘mungiki’ group.

We were remanded for five months then later released.

We are wondering how we are going to solve this problem as it is becoming rampant. If they find a group of around ten to twenty of us, we cannot escape their harassment.