Goodboy

Advocating For Change

Elimu Ni Ngao ya maisha November 1, 2008

Filed under: Uncategorized — petermwatha @ 10:55 am
Tags: , , , ,

Elimu ni ngao ya maisha, ni  muhimu sana kwa sababu kama mtu hajasoma ni vigumu aweze kuajiriwa.

Mfano ni kwamba, mtu akizuru mitaa mengi, ni jambo la kuhuzunisha kupata vijana wengi wakizurura na kupiga gumzo usio na manufaa hata kidogo. Sio kwasababu, hawana la kufanya, ni kwa vile hawakupata fursa ya kuhitimu masomo na pia wavyele wao hawakutia maanani kuwafunza.

Hata hivyo, kuna mabwenyenye wanaowatumia watoto kwa manufaa zao za ubinafsi, kama vile, kuwabebesha takataka, kuwaambia watafute vitu kama vyuma vya biashara zao ilhali malipo ni duni kabisa.Ni matatizo kama haya yanayowakumba na kuwafanya vijana watoroke nyumbani mwao.

Sio tu kazi ya utumwa, inasababisha  vijana kutoroka makwao, pia utumiaji wa dawa ya kulevya imechangia pakubwa. Wanavyo meza tembe zisizo halali kwa wingi, wengi wao huanza kushiriki katika wizi, iliwaweze kununua hizo dawa na kujikimu kiafya.

Nasisitiza zaidi hili hoja ya,” umuhimu wa masomo,” kwa vile wendani wangu wa kufa na kupotea, waliaga dunia mwaka wa 2006, kutokana na uhalifu tuliokuwa tumezoea kutekeleza ikawa mazoea.

Tulikuwa waporaji mali za watu kwa kuwanyonga na hata kuwajeruhi vibaya sana ili tu , tuweze kuwanyanganya mali zao. Lakini, baada ya wenzangu kufyatuliwa risasi na polisi, niliamua kubadilika, kwa kujitegemea kibinafsi bila ya kuwanyanganya watu vitu vyao.

Sina budi, ila tu kuwashukuru watu wa Undugu Society of Kenya, kwa vile wamejimudu na kujikakamua vilivyo kuyashughulikia mahitaji ya watoto wasiojiweza, sio tu kimaumbile, bali pia kwa kuwapa fursa ya kupata elimu.

Wengi wetu tulikuwa chokoraa kama vile tunavyotambulikana katika miji. Lakini, undugu imetushughulikia vilivyo maishani, kwa sasa, sisi ni sawa na watoto wengine, wawe wa mabwenyenye, bado tuko sawa kimasomo.

Ni tumaini letu ya kwamba, ndoto zetu za maishani zitakuja kuona mwangaza siku za usoni.

Translation

Knowledge is power!

Education is very important because if you are not educated you cannot be employed anywhere. If you walk on the streets you will find many youths who are not educated and others did not complete their education, as a result of parents negligence.

It has become a heavy task for us to get worthwhile jobs, forcing most of us to get involved in shoddy businesses, making us be the slaves of the rich people who end up misusing us for their own selfish benefits

There are those people who mistreat us, by giving us hard tasks to perform, like collecting garbage and collecting plastic containers for recycling purposes. They pay us peanuts, and end up selling the items five times what they pay us.

If we complain, they threaten to throw us in jail or even to stop buying the items from us. Yet they are aware that the little cash they give us is not enough to cater for our daily needs.

More so, drugs has ended up killing the dream of education among the youths. This habit made us steal to an extent of even using violence, so that we could cash in money to go and buy with drugs. We became a public enemy. No one so the need to assist us as a result of our bad behavior.

All in all, a friend in need came, one who could understand us, related with us, was ready to transform our lives to the better.

Without the help of Undugu Society of Kenya, most of the street children would have never ever lived to see the dream of change in their lives.

U ndugu has made us great and we are proud of it, for they have enabled us acquire basic education for free, thus, making us be self reliant. Academically, we can stand on the same platform with children from rich families, a great idea that we never imagined to ever acquire in life.

.


 

Watoto Kuongezeka Kwa Mtaa September 27, 2008

Filed under: Uncategorized — petermwatha @ 11:25 am
Tags: , , ,

Ukitembea kwa mtaa utapata watoto wale wametoroka nyumbani hasa kuko na watu wanatumia watoto kwa njia mingi kama kurokota chuma na kuwamwagia takataka. wanawadaganya na mahali pakulala lakini chakula wanajitafutia wenyewe. kuna matajiri wengi wanatumia wegine vimbaya nikielezea kuhusu hawa watoto kutoka niwajue niko na miaka mbili nikielezea kuhusu hawa watoto kuko na matajili wanawapatia watoto kazi ngumu kama kuwambebesha takataka pia wanawabebeza mizigo mizito ukiangalia zile pesa wanazolipwa haziwezi kuwasaidia kwa sababu wanatumia hiyo pesa kununua madawa kama gumu, sigara vitu zigine nyingi. Nikielezea kuhusu tajiri huyo amechukua watoto ana wadhulumu nigeomba selikali ikaweze kuchukua hatua kali kwa watu ambao wana nyanyasa weigine.

Translation

The Increasing Numbers of Street Children

When you walk around the streets, you see the children who have run away from their homes. There are people who use them in many ways, for example, they use them to collect scrap metal and garbage. They deceive them by saying that they will give them shelter and food. There are the rich who use them very badly also. Since I have known these children for two years, the rich give them hard work, for example, carrying garbage, heavy luggage. If you look at the money which they are being paid, the money cannot help them because they use the money to buy drugs like glue, cigarettes and many other things. If I can talk about the rich man, he has taken children and used them in bad ways. I am pleading to the government to take serious action against those people who are using the children in bad ways and also treating them badly.